29th July 2020

Corona yamgeuza mwalimu kuwa yaya

Estimated reading time: 4 minute(s)

Macrine Otieno, mwalimu katika shule ya msingi ya binafsi ya Chrives Royal, jijini Nairobi, ameangua kilio baada ya kujitosa kuajiriwa kazi za uyaya kufuatia maji ya ugumu wa maisha kumfika shingoni kwa yeye na mwanae kukosa hadi chakula, mwenye nyumba kufunga alipokuwa amepanga na baadaye kumtupia vyombo vyake nje kwa kushindwa kulipa kodi.

Kazi ya uwalimu ameifanya kwa miaka sita.

Akizungumza na BBC, mwalimu huyo amesema lockdown ya corona ndicho chanzo cha yote kwani mishahara shule binafsi ilisitishwa, akiba aliyokuwa nayo aliitumia ikaisha na kumsababishia ampeleka mwanae akae na rafiki yake ili akafanye kazi za ndani lakini muda haukupita rafiki yake akampigia simu akamchukue mwanae.

Kwenye kazi za ndani hakupewa uhuru wa kutokatoka, bahati alifanikiwa kuongea na mmoja wa ndugu zake ampeleke mtoto kwa wazazi wake baada ya upenyo wa mipaka ya ndani kufunguliwa kufuatia kufungwa kwa corona.

Amesema mshahara wa ‘housegirl’ akipata anataka kuacha kazi hiyo ili afungue kijimradi chochote.

Tayari BBC wametoa taarifa kuwa amewaeleza tayari ameacha kazi hiyo baada ya kupewa mshahara wake.

Waliomtafutia kazi hiyo ya ndani wamekiri kupokea walimu wengine wanne wakitafuta kazi za ndani ambapo watatu walipata lakini mmoja alikuwa bado kupata sababu ya umri wake kuwa mkubwa, 45.

Hits: 54

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Translate »
Contact VashMedia for right click rights or subscribe!