4th June 2020

Diamond atangazwa nambari mbili Afrika maarufu zaidi YouTube

Estimated reading time: 3 minute(s)

Msanii wa nyimbo za Bongo, Naseeb Abdul maarufu ‘Diamond Platnumz’ ameweka historia baada ya kutajwa kuwa yeye ni msanii nambari mbili kwa mafanikio barani Afrika kupitia mtandao wa Youtube. 

Kwa mujibu wa Jarida la Billboard nchini Marekani, msanii huyo ni mmoja kati ya wasanii wanaotumia vizuri mtandao wa Youtube kufanya mziki na unatazamwa sana.

Tanzania's Diamond Platnumz banned from performing - BBC News

Msanii namba moja anayefanya vizuri kwenye mtandao huo ni Burna Boy kutoka Nigeria huku nafasi ya tatu ikishikwa na Davido kutoka Nigeria. 

Meneja wa Youtube, Kevin Meenan ameeleza kushangazwa na mafanikio ya Diamond ambaye ana wafuasi milioni 3.6 ambao ni sawa na asilimia 80 ya wanaotazama video zake wanatokea nje ya Tanzania. 

Baada ya kupata taarifa hiyo Diamond alitumia kurasa zake za mitandao ya kijamii na kusema ‘Kufanya kazi kwa bidii, kusali na kujiamini ndio siri iliyojificha nyuma yake.’ 

Hits: 134
Follow, like us on social media..

1 thought on “Diamond atangazwa nambari mbili Afrika maarufu zaidi YouTube

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Translate »
Contact VashMedia for right click rights or subscribe!