6th May 2020

Mafuriko yaua 194 Kenya

Estimated reading time: 3 minute(s)

Jumla ya watu 194 wameaga dunia kutokana na mafuriko, kufuatia mvua kubwa inayoendelea kunya sehemu tofauti-tofauti nchini. Haya yamedhibitishwa naye Waziri wa Ugatuzi na Sehemu Kame, Eugene Wamalwa.

Akiwahutubia wanahabari jijini Nairobi, Wamalwa amesema watu zaidi ya 100,000 wameachwa bila makao baada ya mafuriko kusomba maboma na mali yao, huku sehemu tofauti kaunti za Busia, Kisumu, Garissa, Tana-River, Elgeyo-Marakwet, Nyeri na Pokot Magharibi zikiathirika. Kufikia sasa, jumla ya kaunti 29 kati ya 47 zimeathirika.

Serikali imewataka wote wanaoishi sehemu tambarare, kando ya mito na sehemu za chini, kuhamia nyanja za juu ili kuepuka gadhabu ya mafuriko na kuokoa maisha yao, la sivyo wafurushwe kwa lazima.

Alikua ameandamana na Waziri wa Mambo ya ndani Fred Matiang’i, Waziri wa Mazingia Keriako Tobiko, wa Maji, Sicily Kariuki na wa Nishati.

Hits: 232

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Translate »
Contact VashMedia for right click rights or subscribe!