7th June 2020

Nimewajengea wazazi na kupata gari la ndoto yangu – Mbosso

Estimated reading time: 5 minute(s)

Kwa mujibu wa taarifa za Ijumaa/globalpublishers Mbosso tayari ana nyumba ya kisasa ambayo ni ya ghorofa anayoishi mwenyewe jijini Dar es Salaam na pia amewajengea mjengo mwingine wazazi wake.

Lakini kama hiyo haitoshi, star huyo anamiliki gari aina ya Toyota Prado ambalo ni moja kati ya magari ya ndoto yake.

Mbosso na familia yake.

Mbosso mwenyewe alipotafutwa na gazeti hilo alifunguka zaidi kuhusu mafanikio yake ya ghafla baada ya kuwa chini ya WCB.

“Mimi nilikuwa mtu wa ibada sana, nimeswali sana, hata ukiwauliza wenzangu tuliokuwa pamoja Yamoto Band, watakwambia hilo, nakumbuka hata kipindi cha Mfungo wa Ramadhani nilikuwa nakwenda kukutana na watu kwa ajili ya kufanya ibada.

“Naamini nimepewa kipaji cha kutafuta riziki, kwa nini nipishane na kuwa karibu na Mola wangu, niliwahi kumwambia rafiki yangu mmoja hivi, natamani siku moja tupate nyumba ambayo tutakaa kila mtu chumba chake maana tulikuwa tunakaa chumba kimoja tu, kweli Mungu akajaalia tukahamia Tegeta (Dar) nikapata gari pia.

“Nikamwambia pia natamani nimalizie nyumba ya wazazi wangu, natamani wapate gari ya familia, nikimaliza yote hayo natamani kuendesha Prado, nakumbuka kuna kipindi cha Ramadhani ilikuwa usiku nilikwenda kuswali nikiwa na bro wangu Jay Mo, nikaswali na nikaomba Mwenyezi Mungu anitimizie baadhi ya ndoto zangu, anipe hekima na busara kwa viongozi wangu, niwe mwenye kukumbuka nilikotoka, nisiwasahau watu walionisaidia, nisiwe mshamba wa mafanikio, anipe nguvu za kuwasaidia wazazi wangu, yaani huwa namuomba Mungu vitu vingi sana.

“Kwa mwaka jana sikufanikiwa kutimiza ndoto zangu, ila kwa mwaka huu namshukuru Mwenyezi Mungu kanijaalia nimeweza kuwakabidhi wazazi nyumba japo kuna vitu hatujamalizia, nimewapa gari ambalo nina imani litawasaidia, maana familia kubwa watoto tuko wengi na wajukuu wengi kidogo, hata wakipata safari yoyote wanatosha kwenye gari,’’ alisema Mbosso, staa wa Ngoma ya Shilingi.” Ijumaa/globalpublishers.

By SwahiliWorld

Hits: 171
Follow, like us on social media..

1 thought on “Nimewajengea wazazi na kupata gari la ndoto yangu – Mbosso

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Translate »
Contact VashMedia for right click rights or subscribe!