4th May 2020

Wabunge Taita Taveta wataka wakaazi kufaidika na mchango wa kitaifa wa Covid-19

Estimated reading time: 4 minute(s)

Wabunge wa kitaifa kutoka kaunti kaunti ya Taita Taveta wanaitaka kaunti hiyo kuwekwa kwenye mpango wa kufaidika na fedha walizochangisha kwa mujibu wa kuwasaidia wanaoathirika na janga la Covid-19 nchini.

Wakiongea hii leo walipowasilisha mchango wao wa bidhaa za vyakula mbele ya kamati ya County Covid-19 Resource Mobilization mjini Voi, wajumbe hao wakiongozwa na mbunge wa Voi Jones Mlolwa walieelezea hofu waliyonayo ya walengwa kutofikiwa na msaada huo baada ya kamati ya CCRMT kudokeza kupungukiwa na bidhaa wanazokusanya, wiki moja tu baada ya zoezi la ugavi wa chakula hicho kuanza rasmi.

Image may contain: one or more people, sunglasses, cloud and outdoor

Mbunge wa Wundanyi Danson Mwashako, aidha, amewataka waumini wa dini ya kiislamu kutilia maanani maagizo ya wizara ya afya nchini na shirika la WHO kuhakikisha wanasalia salama msimu huu wanapoendelea na maombi ya mfungo wa Ramadhani.

Kwasasa mwenyekiti wa County Covid-19 Resource mobilization Team Ashok Anand amewataka wahisani kujitolea ili kuokoa hatari inayowakodolea macho ya chakula kukosekana.

Image may contain: one or more people and outdoor

Mheshimiwa Mlolwa alitoa bela 70 za unga wa mahindi zikiandamana na mafuta ya kupikia huku Mwashako akitoa mchango sawia na huo kwa kamati ya CCRMT.

Zaidi ya familia 2,000 kutoka mjini Voi zinatarajiwa kupata msaada huo hapo kesho.

Hits: 91
Follow, like us on social media..

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Translate »
Contact VashMedia for right click rights or subscribe!