18th May 2020

Wafanyakazi Marsabit wadai mshahara

Estimated reading time: 3 minute(s)

Wafanyikazi katika kaunti ya Marsabit hawajalipwa mshahara wa mwezi uliopita kutokana na pesa kucheleswa kutolewa na serikali kuu.

Kwa mjibu wa gavana wa kaunti hiyo, Mohamud Ali Mohamud, maafisa wa serikali ya kaunti wamekuwa wakikita kambi katika afisi za wizara ya fedha ili kuhakikisha kwamba pesa zao zinatolewa.

Gavana Ali ameelezea changamoto ambazo hushuhudiwa kucheleshwa kutoa pesa hali ambayo husababisha serikali kupeana zabuni kwa wanakandarasi kabla ya kulipwa baadaye.

Amesema kwamba hata pesa ambazo wananchi wamekuwa wakitaka wapewa badala ya pesa, bado hawajapokea, ila wamepeana zabuni hiyo kwa wanakandarasi ambapo watalipwa baadaye.

Ikumbukwe kwamba wahudumu wa afya ni miongoni mwa wathiriwa wakuu kwa sasa kutokana na kucheleweshwa kwa pesa hizo, ikizingatiwa kwamba kwa hii sasa wanatoa hudumu muhimu Zaidi kukabiliana na virusi vya Corona.

Hits: 163

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Translate »
Contact VashMedia for right click rights or subscribe!