8th May 2020

Waliotoroka Old Town wataona cha mtema kuni, aonya Joho

Estimated reading time: 3 minute(s)

Maafisa wa afya, pamoja na wa usalama kwenye kaunti ya Mombasa, wako mbioni kuwatafuta waathiriwa watano wa virusi vya korona, wanaosemekana kutoroka eneo la Old Town masaa mchache tu baada ya serikali kupiga marufuku kuingia na kutoka eneo hilo, Jumatano wiki hii.

Kulingana na Gavana wa Mombasa Hassan Joho, watano hao ambao bado hawajulikani, walitorokea kusikojulikana na kuwa walikua miongoni mwa kundi la watu 65 waliopimwa virusi hivyo hatari.

Hata hivyo, Joho ameonya kuwa watano hao na yeyote atakayesambaza virusi vya korona makusudi, atachukuliwa sheria.

“Watu watao waliokuwa na virusi vya korona baada ya kuoimwa, walitoroka kutoka Old town na wanajificha badala ya kujitokeza kupata matibabu. Wamsaidia nani? Umeweka hatarini maisha ya wakoo wako,” alisema Joho, Alhamisi, huku akiwataka warejee makwao na kujipeleka hospitalini kupata matibabu la sivyo wajue cha mtema kuni.

Hits: 223
Follow, like us on social media..

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Translate »
Contact VashMedia for right click rights or subscribe!